Huenda sekta ya utalii nchini na hususan eneo la Pwani ikaimarika zaidi iwapo wadau katika sekta hiyo watazidisha juhuzi na kuboresha zao.
Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho alisema kuwa kaunti ya Mombasa imepanga mikakati mwafaka pamoja na kushirikiana na wadau katika sekta hiyo kuhakisha kuwa utamadamu wa mpwani unatambulika.
Alisema kuwa kutokana na kisawa cha Mombasa kuwa na maadhari mazuri ya kuvutia watalii na wageni mbalimbali wanaonuia kuzuru kisiwani kuna haja ya kuwepo na ubunifu zaidi wa kuboresha sekta hiyo.
Aliwataka viongozi wa sekta hiyo kaunti ya Mombasa pamoja na wadau wa sekta ya utalii kushirikiana na kufanya vikao vya majadiliano vitakavyoekeza zaidi sekta hiyo na kukuza uchumi wa kaunti hiyo na taifa la Kenya kwa jumla.
"Chamsingi ni kuhakikisha kuwa tunashirikiana na wadau wote wa sekta ya utalii kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inaboreshwa zaidi na kuwavutia watalii wengi ili kuna kuwa uchumi wa kaunti yetu unaimarika," alisema Joho wakati akiwahutubia wakaazi wa Mombasa siku ya Jumanne.
Kauli ya gavana hiyo inajiri huku maafisa wa Wizara ya utalii nchini pamoja na wadau wengine wakiendeleza mchakato wa kuliuza taifa la Kenya kitalii katika mataifa magharibi ikiwemo Uingereza, Marekani, Sychelles na Uropa.