Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho huenda akajikuta taabani baada ya kukaidi kurudisha silaha anazomiliki licha ya kuagizwa na idara ya usalama kufanya hivyo.

Joho aliyeonekana kukaidi kurudisha silaha hizo, amesema kuwa bastola moja aliyorudisha siku ya Jumamosi ndio aliyopewa wakati alipoingia kuwa gavana lakini silaha zingine alipewa wakati alipokuwa mbunge.

Amesema kuwa ako tayari kushirikiana na maafisa wa usalama lakini hapendi kudhalilishwa kama kiongozi kwani alichaguliwa na wananchi na wala hakupewa uteuzi wa moja kwa moja ili kuongoza kaunti ya Mombasa.

"Niko tayari kushirikiana na maafisa wa usalama kuimarisha usalama wa kaunti ya Mombasa lakini kudhalilishwa sitakubali kama ni bastola nimepeya nilizopewa nikiwa gavana lakini zilizopewa kama mbunge hizo sioni nikitoa sasa, serikali lazima izingatia maisha ya wananchi," alisema Joho  siku ya Jumatatu mjini Mombasa.

Kushinikizwa kwa gavana joho kurudisha bastola yake kwa maafisa wa polisi kumejiri baada ya mshirikishi mkuu wa utawala eneo la Pwani Nelson Marwa kuagiza walinzi wa viongozi hao kurudishwa kambini kutokana na utumizi mbaya wa mamlaka yao.

Waziri wa usalama wa ndani nchini Joseph Nkaissery amesisitiza kurudishwa kwa silaha hizo na iwapo viongozi waliyogiza watakaidi basi watachukuliwa hatua za kisheria.