Share news tips with us here at Hivisasa

Naibu wa rais amesema kuwa serikali ya Jubilee itaendea kuwaunganisha Wakenya wote pasi kujali dini wala kabila, kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Akizungumza siku ya Jumatano huko Malindi, William Ruto alisema kuwa ni jukumu la serikali kuhudumia wananchi pasi ubaguzi wowote ule, kama katiba inavyoagiza.

Aidha, alisihi viongozi wanaoendeleza siasa za ukabila na ubaguzi kuasi siasa za aina hiyo na badala yake kuwaunganisha Wakenya kuwa kitu kimoja.

Akiendeleza kampeni zake kwa siku ya pili huko Shella mjini Malindi, Ruto alisema serikali haitowabagua wananchi, na kwamba wakaazi wa Malindi wanahaki ya kupata maendeleo kutoka kwa serikali licha ya kuwa eneo hilo halikupigia kura serikali ya Jubilee katika uchaguzi mkuu uliopita.