Share news tips with us here at Hivisasa

Kinara wa mrengo pinzani Raila Odinga amedai serikali ya Jubilee imeshindwa kuliongoza taifa.

Akizungumza siku ya Jumatano jijini Mombasa wakati wa uzinduzi wa barabara ya Fidel Odinga katika eneo la Kengeleni, Odinga amesema Jubilee imeshindwa kukabiliana na tatizo sugu la ufisadi.

Odinga alidai serikali ya Jubilee imeshindwa kutekeleza ahadi walizotoa kwa wananchi wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2013.

Aidha, alitaja mkopo wa dhamana ya Eurobond kama sakata kubwa ya ufisadi inayoiandama serikali hiyo kushinda sakata ya Anglo Leasing na Goldenberg.

Raila aliongeza kuwa Rais Kenyatta anawahadaa wakenya kupitia miradi inayofadhiliwa na mashirika ya kimataifa, akitolea mfano mradi wa Mwangaza Mitaani uliofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia serikali ya Kaunti ya Mombasa.