Share news tips with us here at Hivisasa

Mkutano wa viongozi wa wanafunzi wa chuo cha kiufundi cha Mombasa na kamati ya kaunti ya Mombasa ulikosa kufanyika kwa sababu ya ukosefu wa mawasiliano ya kutosha.

Kiongozi wa wanafunzi hao Ocharo Ondiek alisema siku ya Jumatau kuwa hawakuweza kuelewana na kamati ya kaunti kwa sababu za kiitifaki, na sasa mkutano huo utafanyika Ijumaa

Lengo kuu la kikao hicho lilikuwa kuajadili malalamiko yaliyosababisha wanafunzi hao kugoma na njia za kufuatwa kwa waliofanya uharibifu wakati wa maandamano hayo.

Mwezi jana, wanafunzi hao waligoma wakilalamikia kuongezwa kwa karo na kunyanyaswa kimasomo, mgomo uliosababisha hasara kubwa baada ya wanafunzi hao kuchoma magari mawili ya serikali ya Kaunti ya Mombasa na kutatiza shughli za uchukuzi.

Katika taarifa iliyochapishwa na chuo hicho na kutiwa sahihi na naibu chansela Joshpat Mwatela, usimamizi wa chuo hicho ulipinga madai hayo na kusema karo ziliongezwa kwa wanafunzi maalum ambapo walizihitaji kwa safari za kimasomo na kulikuwepo na mashauriano kabla ya kuongezwa kwa karo.