Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baraza la manaibu magavana sasa limekubali kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha sintofahamu baina yao na magavana, kuhusu majukumu ya kila mmoja.

Baraza hilo limependekeza kubuniwa kwa kamati ya magavana watano ambao wataketi chini na manaibu wa magavana ambao wanazozana na magavana katika kaunti mbali mbali nchini ili mazungumzo yaanze.

Wakizungumza wakati wa kongamano linaloendelea katika hoteli ya Enashiapi mjini Naivasha, wakuu hao wamesema kuwa mazungumzo hayo yanafaa kufanywa haraka iwezekanavyo.

Manaibu magavana waliozungumza ni pamoja na Gitonga Kabugi, Waithaka Mwangi na Gakure Monyo wa kaunti za Laikipia, Nyandarua na Murang’a mtawalia.

“Wakati mwingine hata hatujui kinachoendelea kwenye kaunti, au tunafaa kufanya kazi ipi, sisi ni kama watu ambao wamo gizani” alisema Gakure Monyo, naibu gavana wa kaunti ya Murang’a.