Kamishina wa kaunti ya Nakuru Joshua Nkanatha amewataka machifu wote kuhakikisha wale wote waliotuma maombi ya vitambulisho vya kitaifa wanapata vitambulisho hivyo. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza afisini mwake, Kamishina Nkanatha amesema kuwa hatua hiyo ni njia mojawapo ya kuimarisha usalama. 

Anasema kuwa wengi wa wahalifu hukosa kujulikana kwa vile hawana vitambulisho na wale wasio na vitambulisho wanafaa kufanya hima. 

Wakati huo huo amewaonya wahalifu katika kaunti ya Nakuru kwamba vyuma vyao vi motoni.

"Kama kuna mtu anataka kujaribu kusumbua utulivu uliopo ajue siku zake zimewadia kwani tuko macho hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu," alisema Nkanatha. 

Wakati huo huo ametoa wito kwa wazazi kupima mienendo ya watoto wao.

Kwa mujibu wake, watoto wengi hujiingiza katika makundi haramu kutokana na wazazi kuwatelekeza. 

 PHOTO CAPTION:

Kamishina wa Nakuru Joshua Nkanatha akiwa afisini. Amewataka machifu kuhakikisha kila aliyetimu miaka 18 anapata kitambulisho.PRISTONE MAMBILI/Hivisasa.com