Share news tips with us here at Hivisasa

Kamishna mkuu wa wakfu wa kiislamu ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa Nacada tawi la Mombasa Sheikh Juma Ngao amekiri kuwepo na kukithiri ufisadi katika wakfu huo, jambo alilolitaja kama ufujaji wa mali ya umma.

Akihutubia wananchi katika sherehe ya Jamuhuri siku ya Jumamosi katika uwanja wa Tononoka jijini Mombasa, Ngao alionyeshwa kusikitishwa kwake na kukashifu vikali jinsi fedha za umma zinavyofujwa bila kujali, na kusisitiza kuwa hatua hii inalemaza uchumi wa taifa.

Sheikh Ngao ameapa kupinga ufisadi unaoghubika tume hiyo, akikariri haja ya kujitolea kwake kuhusiana na swala hilo.

Aidha, ametaka idara husika kuwajibika katika kupiga vita ufisadi nchini, na kusisitiza watakaopatikana na hatia wakabiliwe kisheria.

Aidha, Ngao aliwahimiza wabunge kuhakikisha kuwa wanatumia fedha wanazozipokea kuhakikisha wanapigana na mihadarati katika maeneo yao, kama njia moja ya kuhakikisha maisha bora kwa vijana.