Huku wakenya wakizidi kuomboleza vifo vya wanajeshi waliuawa wiki jana katika shambulizi la Alshabaab, Kasisi George Wamani wa dhehebu la PCEA Dkt Arthur Nakuru ametoa wito wa maombi kwa ajili ya familia zao.
Akizungumza Jumapili wakati wa ibaada katika kanisa hilo, Kasisi Wamani amesema kuwa wakati huu wa majonzi ni vyema wakristo na wakenya kwa jumla kukumbuka vikosi hivyo na familia zao.
"Ni wakati huu ambapo tunafaa kuombea vikosi vya usalama na hata familia zao," alisema kasisi Wamani.
Wakati huo huo ametoa wito kwa wakristo kukumbuka familia zote katika maombi akisema msingi bora wa taifa ni familia.
"Tunajua kuna changamoto kadhaa za kifamilia humu nchini lakini hatufai kufa moyo bali tuzidi kuzikumbuka katika maombi," aliongeza Kasisi Wamani.
Wakati wa ibada hio ya Jumapili katika Dhehebu hilo la PCEA Dkt Arthur, mchango maalumu ulifanywa kwa ajili ya wasiyojiweza katika jamii wakiwemo wakongwe.