Maafisa wa afya kaunti ya Nyamira wameonya vikali dhidi ya mazoea ya kuiba madawa kutoka zahanati na hospitali mbalimbali ili kuyauza. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubu siku ya Alhamisi alipoitembelea zahanati ya Nyaiguta siku ya Alhamisi Katibu wa afya kwenye kaunti hiyo Douglas Bosire alionya kuwa idara ya afya itaanzisha udadisi kubaini jinsi dawa zinavyoibiwa na kisha kuwatia mbaroni watakao patikana na hatia. 

"Nataka kuwahakikishia kuwa serikali ya kaunti hii imenunua dawa za kutosha na inashangaza na ni vipi hospitali na zahanati mbalimbali hazina dawa ila tumeanzisha uchunguzi kuwakabili wanaohusika," alionya Bosire. 

Bosire aidha alisema kuwa wataanzisha msako kwenye duka zinazouza madawa zinazomilikiwa na wahudumu wa afya na zinazokisiwa kuuza dawa za wizi zilizonunuliwa na serikali ya kaunti hiyo ili kuwatia mbaroni washukiwa.

"Kama serikali hatuwezi vumilia tabia ya watu wachache kutumia mamlaka yao kuwanyanyasa wananchi kwa kuwanyima haki ya kupata huduma bora ya matibabu kwa kuwa tunajua baadhi ya watu wanaomiliki duka za kuuza dawa zinazo kisiwa kuibwa kutoka kwenye hospitali na zahanati za serikali, na naonya wajitokeze mara moja kabla tuwatie mbaroni," alisisitiza Bosire.