Serikali ya Kaunti ya Kisii imeombwa kupunguza bei ya dawa katika hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii iliyoko mjini Kisii.
Kulingana na wagonjwa ambao walienda kutafuta na kupata huduma ya matibabu katika hospitali hiyo, gharama ya dawa katika hospitali hiyo iko juu mno ikilinganishwa na hospitali zingine za kibnafisi.
Wito huo umetolewa kwa serikali ya kaunti hiyo ili kutoa usaidizi wa kupunguza bei ya dawa hizo zinazouzwa katika hospitali hiyo.
Wakiongea na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumanne katika hospitali hiyo, wakazi waliowaleta wagonjwa kutibiwa katika hosptali hiyo walisema bei ya dawa imepanda zaidi ikilinganishwa na hospitlri zingine za kibinafsi .
“Mgonjwa wangu amehudumiwa kimatibabu sasa tumetumwa kununua dawa kutoka duka hili la kuuza dawa lakini bei ya dawa tumeambiwa ni ya juu zaidi, tunaomba tupunguziwe bei,” alisema Richard Nyangeri, mkazi aliyemleta mgonjwa.
Juhudi za waandishi wa habari za kuwahoji madaktari kuhusu madai hayo zilifua dafu, lakini wakaelezwa bei ya dawa huwa inapadilika kila kuchao na hawana la kupunguza kwani kutakuwa na hasara.
Sasa serikali ya kauti imeombwa kuingilia kati kuwapunguzia mzigo wakazi, kwani gavana wa kaunti hiyo James Ongwae aliahidi kuimarisha sekta ya afya zaidi Kisii.