Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kaunti ya Mombasa imebuni mfumo wa digitali wa kunakili shughuli zote za kaunti za ukusanyaji ushuru kutoka kwa umma ili kukabiliana na maafisa wa kaunti wanaoshiriki ufisadi. 

Kaimu mkurugenzi mkuu wa Maaskari wa kaunti ya Mombasa Charles Changawa amesema kuwa mfumo huo kwa kiasi kikubwa umepunguza kashfa za ufisadi kwenye idara mbalimbali za kaunti hiyo.

Kwenye mahojiano ya kipekee na mwanahabari wetu afisini mwake siku ya Jumatano, Changawa amesema kuwa juhudi hizo ni za kuhakikisha kuwa mali ya umma inalindwa vyema na wale watakaopatikana wakishirki ufisadi watachukuliwa hatua za kisheria.

"Tumebadili mfumo mpya wa kutumia digitali kuhakikisha kuwa kashfa zote za ufisadi hazitatokea katika afisi zetu ili kuona kuwa mali ya umma hasa ukusanyaji ushuru unatakelezwa vyema bila ufisadi," alieleza Changawa.

Wakati uo huo Changawa amesema kuwa maaskari wa kaunti kwa ushirikiano na maafisa wa polisi katika kaunti ya Mombasa wanashika doria kikamilifu kuhakikisha kuwa masuala ya usalama yanaimarishwa.