Kaunti ya Nakuru imeorodheshwa kati ya kaunti zilizosajili maambukizi mengi mapya ya virusi vya HIV na ugonjwa wa ukimwi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hayo yalibainika wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya ukimwi ulimwenguni zizlizofanyika katika bustani ya nyayo mjini Nakuru.

Kulingana na ripoti ilyiotoewa na baraza la kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchini (NACC), Nakuru ilisajili visa elfu nne vya maambukizi mapya ya HIV katika kipndi cha mwaka mooja uliopita.

Mshirikishi wa NACC kanda ya bonde la ufa Hillary Chepsiror alisema kuwa idaid hiyo ni kubwa zaidi ikilinganishwa na kaunti zingine nchini.

Chepsiror alisema kuwa zaidi ya watu elfu sitini na siat wanaishi na virusi vya HIV katika kaunti ya Nakuru huku wengi wakiwa katika maeneo ya miji ya Nakuru, Gilgil, Naivasha, Maai-Mahiu na Salgaa.

“Inasikitisha kuwa Nakuru inaongoza kwa kusajili visa vingi vipya va maambukizi ya HIV na kati ya visa hivyo elfu nne vijana na watu wenye umri wa makamo ndio wengi sana,” akasema Chepsiror.

Maambukizi mengi yametokea katika maeneo ya mji haswa katika barabara na vituo vya kibiashara kulingana na afisa huyo.

Chepsiror alisema kuwa baraza la kukabiliana na ukimwi nchini limeandaa mkakati wa miaka mitano wa kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi katiak maeneo ya Salgaa,Nakuru,Naivasha na Maimahiu.

“NACC inatilia mkazo juhudi zinazofanywa na mashirika ya kijamii katika maeneo haya kukabili janga hili ma tutafanya kazi nao ili kuhakikisha kuwa visa hivi vinapungua,” akasema.