Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kaunti ya Nyamira imelaumiwa vikali kwa kutonunua zima moto kwa kaunti hiyo.

Hii ni baada ya moto kushika maduka ya mji wa Kebirigo na kuharibu mali ya dhamani kubwa.

Akizungumza siku ya Jumapili wakati kisa hicho kilichotokea mjini Kebirigo mwakilishi wa wadi ya Bonyamatuta Robinson Mocheche alilaumu serikali kwa kuchukua mda mrefu bila kununua zima moto.

Mocheche alisema bunge la kaunti hiyo ilitenga pesa katika bajeti ambazo zingetumika kununua magari ya kuzima moto lakini hadi sasa serikali hiyo haijanunua gari ata moja.

“Ninalaumu serikali kwa kutojali maslahi ya wananchi wanapokumbwa na mkasa wa moto, sisi wawakilishi wa wadi tulitenga pesa katika bajeti ambazo zingetumika kununua gari la kuzima moto lakini hadi sasa hakuna gari limenunuliwa na hiyo si haki,” alisema mwakilisdhi Robinson Mocheche.