Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Kaunti ya Kisii imeombwa kuanzisha hazina ya mayatima kwa kila wadi ili kusaidia mayatima kujiendeleza kimasomo na kujiimarisha kimaisha.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa idadi kubwa ya mayatima katika sehemu za mashinani hawajawahi kunufaishwa na serikali ya kaunti hiyo ili kuwafadhili kujiendeleza kimasomo kwani huwa vigumu kufikiwa, jambo ambalo limelazimu serikali hiyo kuombwa kuanzisha hazina hiyo kwa kila wadi ili wawakilishi wadi wawe wanatoa usaidizi kwa mayatima hao.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu katika mji wa Marani, wakazi wa eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini wakiongozwa na John Masiita waliiomba serikali ya Kaunti ya Kisii kutoa usaidizi kwa mayatima katika sehemu za mashinani kupitia kuanzishwa kwa hazina hiyo ya mayatima.

“Idadi nyingi ya mayatima katika sehemu za mashinani hawajawahi faidika na serikali ya kaunti kujiendeleza kimasomo na ata kimaisha kwa kufadhiliwa ili kufanya biashara,” alisema Masiita

“Tunaomba serikali ianzishe hazina ya mayatima kwa kila wadi maana tunaona wengi wao wamejitenga na shule kufuatia ukosefu wa pesa na wengine husumbuka katika vijiji mbalimbali,” alisema Ketty Bosibori, mkazi mwingine.

Jukumu ni la serikali ya kaunti hiyo kuitikia wito huo ambao umeonekana kuwa na uzito ili mayatima kusaidiwa katika vijiji mbalimbali