Share news tips with us here at Hivisasa

Baada ya serikali ya Kaunti ya Kisii kutenga sehemu ya uwanja wa mapumziko mjini Kisii, sasa serikali hiyo imeombwa kuharakisha ukarabati wa uwanja huo.

Hii ni baada ya uwanja huo kusalia bila kukarabatiwa kwa muda mrefu, huku wakazi wakiendelea kungoja uwanja huo kukarabatiwa bila kuona matunda ya ukarabati kuanza.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne mjini Kisii, wakazi wa kaunti hiyo, wakiongozwa na Lydia Bochaberi na Evans Mireri waliomba serikali kuwakarabatia uwanja huo uliotengwa hapo awali ili wakazi wawe wanapumzikia katika uwanja huo baada ya uchovu wa kazi.

Kulingana na wakazi hao, wanahitaji uwanja huo kwa kutoa maombi kwa serikali ya kaunti hapo mbeleni na serikali ikaitikia wito wao huku wakiomba msaada wa uwanja huo kukarabatiwa kikamilifu ili wawe wanapumzikia.

Wakazi hao walisema hawawezi kupumzikia uwanja huo ambao hauna pahali pa kukaa kutokana na ukosefu wa ukarabati huku nyasi zikiwa kubwa na kudai huenda nyoka zimeweka makao yao kwa uwanja huo.

“Tunaomba serikali yetu ya kaunti kuitikia ombi letu na kuharakisha kukarabati uwanjwa wa mapumziko ili kukamilisha ukarabati wa uwanja huo,” alisema Bochaberi.

“Katika uwanja huo kuna nyasi kubwa na hatuwezi kupumzikia hapo ingawa tunahitaji kupumzika baada ya kazi kwani twahofia kuwa huenda nyoka wameweka makao yao mle ndani ya uwanja,” aliongeza Bochaberi.