Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwenyekiti wa chama cha sauti ya wajane katika Kaunti ya Kisii Magret Obiri ameiomba serikali ya kaunti kuhusisha wajane katika miradi ya maendeleo ili nao waweze kujiendeleza na kujiimarisha kimaisha.

Kulingana na Obiri, idadi kubwa ya wajane hawahusishwi katika miradi ya maendeleo inayofanywa na serikali ya kaunti, na kupelekea kusema wanabaguliwa.

Akizungumza siku ya Jumanne mjini Kisii, Obiri alisema ni haki kwa wajane kuhusishwa katika miradi ya maendeleo kama watu wengine wa kawaida.

Pia Obiri alisema mara nyingi wajane hawasikikiki kufuatia 'kutoshikwa mikono' na serikali, na kusema hawana nguvu ya kujitetea maana hakuna wa kuwasaidia.

“Sisi wajane mara nyingi tunabaguliwa kwa serikali, tunaomba serikali ya kaunti yetu inayoongozwa na Gavana James Ongwae iweze kutuhusisha kwa miradi ya mandeleo ili tuweze kujiendeleza kimaisha,” alisema Obiri.

Aidha, mwenyekiti huyo alisema wanapotafuta huduma kwa ofisi za seriali hubaguliwa zaidi, jambo ambalo limewashangaza na kuwakera wengi na kuomba msaada utoka kwa serikali.

“Mama ambaye ni mjane anapopata shida yoyote anapotafuta usaidizi haswa kwa ofisi ya chifu anabaguliwa, na hilo limekita mizizi katika Kaunti ya Kisii. Tunaomba hilo liweze kukomeshwa tuko sawia na wengine,” aliongeza Obiri.

“Tunaomba tunapoenda ofisi yoyote tuweze kupata huduma kama wengine maana nasi ni binadamu,” alisistiza Obiri.