Serikali ya kaunti ya kisii imeombwa kutenga shamba hekari 200 kwa ujenzi wa viwanda katika kaunti hiyo ili kuinua sekta ya biashara na kuinua uchumi wa kaunti hiyo pamoja na taifa lote la Kenya kwa ujumla.
Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa katika kaunti ya kisii hakuna viwanda huku ikionekana biashara kuendelea kupanda zaidi katika kaunti hiyo kila kichao.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika kongamano la wafanyibiashara katika chuo kikuu cha kisii mjini kisii katibu wa wizara ya viwanda Ali Mohamed alisema ikiwa kaunti ya kisii inahitaji kujiendeleza zaidi katika biashara na kuinua uchumi sharti itenge shamba kwa ujenzi wa viwanda mbalimbali katika kaunti hiyo.
“Naomba serikali ya kaunti ya kisii kutorudi nyuma katika biashara kwani ina mazao mengi ambayo yanaeleta manufa kwa wakazi wa kaunti hii,” alisema Ali Mohamed .
“Pia Naomba serikali hii ya kaunti kupitia gavana James Ongwae kutenga shamba hekari 200 ili viwanda kujengwa na kuinua biashara maana wawekezaji hapo ndio huwekezazaidi kwa biashara,” aliongeza Mohamed.
Kwa upande wa gavana wa kisii James Ongwae alisema serikali yake itahahakisha biashara vitaendelea kuinuka zaidi ili kunufasha wengi kujiendeleza kimaisha.
Mkutano huo ulihudhuriwa na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga ambaye alifungua kongamnao hilo rasimi, seneta wa kaunti ya kisii Chris Obure, naibu gavana wa kisii Joash Maangi na wengine.