Serikali ya kaunti ya Kisii imeombwa kuhakikisha kutimiza ahadi za kujenga maktaba katika kila eneo bunge jinsi ilivyoahidi hapo mbeleni.
Hii ni baada ya serikali hiyo kutangaza kujenga maktaba hizo kwa maeneo bunge yote tisa, jambo ambalo limechukua muda mrefu na halijatimizwa hadi sasa.
Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatano mjini Kisii, wakazi hao waliomba serikali kujenga maktaba hizo ili kufadhili zaidi masomo kwa wanafunzi wa kaunti hiyo.
“Tangu serikali hii ituahidi kutujengea maktaba za vitabu katika kila eneo bunge la kaunti hii hatujaona chochote kikifanyika,” alisema Mattews Kerama, mkazi.
“Tunaomba maktaba hizo ziijengwe ili wanafunzi wetu kusoma zaidi kwa kufika kwa maktaba hizo na kusoma ili elimu kunoga zaidi hapa Kisii,” alisema Ombasa Danson mkazi mwingine.
Wakati huo huo, wakazi hao waliomba serikali ya kaunti hiyo kujaribu kila iwezalo kuhakikisha basari zote hutolewa kwa wanafunzi wa shule hutolewa kwa njia ya haki na uwazi bila mapendeleo ili nwanafunzi wote kufaidika kimasomo katika kaunti hiyo ya Kisii ili kuingara kwa masomo.
Picha: Afisi za serikali ya kaunti ya Kisii. Serikali hiyo imeombwa kuhakikisha kutimiza ahadi za kujenga maktaba za vitabu katika kila eneo bunge jinsi ilivyoahidi hapo mbeleni. DennisN/Hivisasa