Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali ya Kaunti ya Kisii imeombwa kuwapa vijana kandarasi ya kusafisha masoko katika eneo bunge la Mugirango kusini ili kujiendeleza na kujiimarisha kimaisha.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu mjini Nyamarambe, vijana wa muungano wa Bogetacha Bomo wakiongozwa na mwenyekiti wao Geoffrey Mengo waliomba serikali ya kaunti kuwapa kandarasi ya kufanya usafi soko moja au mbili katika eneo bunge hilo ili kujiendeleza kwa kupata riziki ya kila siku.

Kulingana na vijana hao, waliunda muungano wao baada ya serikali ya kaunti kutoa ahadi hapo mbeleni kuwa itakuwa ikikabidhi vijana kandarasi ya kusafisha masoko.

“Tuliunda kikundi chetu kama vijana wa eneo hili la Mugirango kusini ili tukabidhiwe kandarasi ya kufanya usafi katika mojawapo ya soko katika eneo hili ili tupate riziki ya kila siku na kujiendeleza,” alisema Mengo.

“Kile kilitufanya tukafiria hivyo, idadi kubwa ya vijana wa eneo hili hawana kazi ya kufanya ili hali serikali ya kaunti ya Kisii ilitangaza hapo mapema kuwa itakuwa ikikabidhi vijana kazi ya kuafisha miji mikuu kama masoko ili kujiendeleza,” aliongeza Mengo.