Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali ya kaunti ya Nyamira imeombwa kuunda  hazina ya mikasa ili kutoa ufadhili kwa watakaoathirika kupitia mikasa ya moto na mikasa mingine ili kujiendeleza.

Wito huo ulitolewa baada ya maduka kadhaa kuteketea mjini Kebirigo usiku wa jumapili na kusababisha hasara kubwa miongoni mwa wafanyibiashara huku hazina ya kusimamia ufadhili zikiombwa kuanzishwa katika kaunti ya Nyamira.

Akizungumza na siku ya Jumanne mjini Nyamira mwenyekiti wa Jomo Kenyatta foundation Walter Nyambati alisema itakuwa vizuri hazina ya mikasa kuundwa ili kufadhili wahusika wanaokumbwa na mikasa ya moto na mikasa mingine na kuomba serikali ya kaunti ya Nyamira kufanya hivyo ili kuokoa wengi wanapopata hasara.

“Naomba serikali yetu ya kaunti ya Nyamira kujali maslahi ya wakazi wa kaunti pindi wanapopata hasara kupitia mikasa ya moto na mikasa mingine inapotokea ghafla,” alisema Walter Nyambati.

“Nadhani hilo likifanywa wengi wanaokadiria hasara watakuwa wakisaidiwa ili kujiendeleza kimaisha kuliko kuendelea kuwa maskini wanapata hasata kupitia mikasa,” aliongeza Nyambati.