Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali ya kaunti ya Kisii imeombwa kuweka mataa katika soko la Kenyenya eneo bunge la Bomachoge kuimarisha usalama zaidi katika soko hilo.

Ombi hilo limetolewa wiki chache tu baada ya serikali hiyo ya kaunti kuweka taa katika soko hilo, lakini wafanyibiashara hao wanaomba kuongezwa kwa taa zingine kwa sababu soko hilo ni kubwa.

Wakizungumza siku ya Jumanne katika soko hilo, wafanyibiashara hao wakiongozwa walisema usalama umedorora zaidi katika soko hilo, na kusema hawawezi kuendelea na biashara zao hadi mwendo wa saa mbili.

Wakati huo huo, wafanyibiashara hao waliomba serikali hiyo ya kaunti kuwajengea vyoo vya kisasa katika soko hilo kuimarisha mazingira

“Serikali ya kaunti yetu imekuwa ikitoa ahadi za kuimarisha usalama kwa kuweka mataa katika soko hili kila wakati lakini ahadi hiyo bado haijatimizwa, tunaomba mataa kuwekwa katika soko hili,” alisema Beatrice Misati, mwanabiashara

“Tunaomba pia kujengewa vyoo ili mazingira ya soko hili yaweze kuimarika zaidi na tufanyiwe maendeleo maana ata barabara ya kuingia katika soko hili bado kukarabatiwa,” alisema Kemunto Ongon’di.