Wafanyibiashara wa soko la ‘Market’ lililoko katikakati mwa mji wa Kisii wameomba serikali ya kaunti ya Kisii kufungua kituo kipya cha magari karibu na soko hilo ili kuinua biashara zao.
Kulingana na wafanyibiashara hao hapo zamani kituo cha magari kilipokuwa karibu na soko hilo biashara vilikuwa kwa kiwango cha juu zaidi baadaye biashara vikarudi chini wakati kituo hicho kilihamishwa kwingine kutoka mahala hapo.
Wakizungumza na mwandishi huyu wa habari siku ya ijumaa katika soko hilo la Market lililoko mjini Kisii wafanyibiashara hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Elijah Ombongi waliomba kituo kimoja cha magari kufunguliwa katika soko hilo.
“Tunaomba gavana wetu wa kaunti ya Kisii James Ongwae atufungulie kituo cha magari karibu na soko letu hapa ili tuone kama biashara zetu vitainuka zaidi hadi kiwango cha zamani,” alisema Elijah Ombongi.
Ata hivyo wafanyibiashara hao waliomba kuongezewa taa moja la kumlika usiku katika soko hilo ili kuimarisha usalama zaidi.
Sasa jukumu ni la serikali ya kaunti ya Kisii kuitikia ombi la wafanyibiashara hao na kufanya yale wanahitaji ili kuwatimizia
Ombongi alisema hii si mara ya kwanza kwa wafanyibiashara hao kuomba gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae fanya hayo lakini wanaendelea kusubiria maendeleo hayo.
caption ya picha
Wafanyibiashara wa soko la ‘Market’ mjini Kisii .Wameomba serikali ya kaunti ya Kisii kufungua kituo kipya cha magari karibu na soko hilo ili kuinua biashara zao[Dennis N/hivisasa.com]