Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kesi iliyofikishwa katika mahakama ya Nyamira kupinga uchaguzi wa viongozi wa chama cha walimu KNUT tawi la Nyamira Imeahirishwa.

Hii ni baada ya viongozi waliochaguliwa kukosa kuwa na mawakili wa kuwatetea na kupelekea kuongezewa mda ili kutafuta mawakili wa kuwatetea

Wawaniaji ambao walipinga uchaguzi huo uliokamilika kwa majuma mawili yaliyopita na kufikisha kesi hiyo kwa mahakama miongoni mwao ni Julius Matwere aliyekuwa anawania kiti cha ukatibu,Charles Ombui aliyekuwa anawania kiti cha uwenyekiti , Cicilia Ondima aliyekuwa anawania kiti cha uakilishi wa wanawake walipinga uchaguzi huo kwa kusema hukuwa wa haki na uwasi.

Kesi hiyo ingesikizwa jana tarehe 29 lakini ukahirishwa na jaji wa mahakama hiyo Chrispene Lagira huku akitoa tarehe mpya ya kusikiza kesi hiyo machi 15, 2016.

caption ya picha

Bango la mahakama  .Jaji wa mahakama ya Nyamira Chrispene  Lagira  aliagiza kesi hiyo kusikizwa tena machi 15, 2016. [DennisN/www.hivisasa.com]