Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Bahati Onesmus Kimani Ngunjiri amepongeza mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kukataa kutumia ushahidi uliokataliwa dhidi ya naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua Arap Sang. 

Akizungumza Ijumaa punde tu baada ya uamuzi huo kutolewa, Ngunjiri amesema kuwa ni dhihirisho kesi hii inaelekea kutamatika. 

Kwa mujibu wake, kiongozi mkuu wa mashtaka katika mahakama hiyo Fatou Bensouda atakuwa na kibarua kigumu na huenda akakosa kesi. 

"Ni bayana kwamba sasa kesi hii inatamatika hivi karibuni na ningependa kushukuru sana mahakama ya ICC kwa uamuzi wa hivi punde," alisema Ngunjiri. 

Wakati uo huo, ametoa wito kwa wananchi kuwa watulivu na kungojea uamuzi wa mwisho kuhusiana na kesi hiyo.