Share news tips with us here at Hivisasa

Kesi ya walimu 12 wa shule ya msingi ya Star of the Sea wanaodaiwa kupatikana na mitihani kinyume cha sheria imehairishwa kusikilizwa baada ya ripoti ya uchunguzi kutoka kitengo cha kuchunguza visa sampuli hiyo, almaarufu 'cybercrime' kutokua tayari.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Februari 18 mwaka ujao.

Novemba 10,2015 walimu hao walipatikana na mitihani ya masomo ya hisabati, kingereza na utungaji katika shule hiyo kabla ya mitihani yenyewe kukaliwa.

Walimu hao walifikishwa mahakamani mwezi Novemba 12, 2015 na kukanusha madai hayo.

Mahakama iliwaachilia kwa dhamana ya shilingi nusu milioni ama dhamana ya pesa taslimu shilingi 200,000, na kungoja kuskizwa kwa kesi hiyo mwaka ujao.