Share news tips with us here at Hivisasa

Kesi inayowakabili wanachama wa vuguvugu la MRC wanaokabiliwa na kosa la mauaji na kuzua vurugu wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013 , imeahirishwa baada ya uamuzi wa kesi kutokuwa tayari.

Siku ya Ijumaa, Jaji Martin Muya aliwaambia washtakiwa hao kuwa uamuzi bado haujakuwa tayari na kupendekeza kutoa uamuzi wake tarehe Machi 23, 2016.

Faraji Konde Kazungu, Omari Diofu Gwashe, Suleiman Mohamed Suleiman na Justus Randu Nyando, wanakabiliwa na madai ya mauaji ya askari Harrison Maitha, aliyekuwa mlinzi wa Gavana wa Kaunti ya Kilifi Amason Kingi mnamo Octoba 4, 2012 katika eneo la Mtomondoni huko Kilifi.

Aidha, wanne hao wanakabiliwa na kosa la kupanga njama ya kuvuruga uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 huko Kilifi.

Vile vile, wanakabiliwa na shtaka la kupanga njama ya kuvuruga mtihani wa kitaifa wa mwaka 2013 huko Kilifi.