Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanachama wa Bunge la Africa Mashariki, ambaye pia ni mbunge wa zamani wa Mugirango Kaskazini Joseph Kiangoi, amesema marekebekisho ya vipengee vya rasimu ya katiba, wanayo pendekeza viongozi wa mlengo wa Cord, yanafaa kujumuisha mageuzi ya kuwa na uongozi wa urais unaojumuisha serikali ya bunge, ili kuepukana na hali ya uongozi wa urais wa sasa.

Akihutubu wakati wakusherehekea miaka 63 tangu kuzaliwa kwake kwenye mkahawa mmoja mjini Nyamira siku ya Jumapili, Kiang'oi alisema kuwa ikiwa hilo litaafikiwa, itakuwa rahisi kwa jamii zilizotengwa kupata nafasi za uongozi, na pia kupunguza kampeni zakuchacha za uwaniaji urais nchini.

"Tayari nimezungumza na kamati ya Okoa Kenya na nimewashinikiza kuhakikisha kuwa wanabadilisha mageuzi ya uongozi wa urais na kuyafanya yawe ya njia ya ubunge kwa kuwa hali hii itazisaidia jamii za Wakenya zilizotengwa kupata nafasi yakuhudumu katika nyadhifa mbalimbali serikalini,” alisema Kiangoi.

Kiong'oi alisema kuwa ikiwa hilo litaafikiwa, basi itakuwa rahisi kwa chama kilichoko na idadi kubwa ya wabunge bungeni kuwa ndicho cha kuunda serikali, chini ya uongozi wa waziri mkuu, hali ambayo itamruhusu waziri mkuu kufanya miungano na vyama vingine vya kisiasa.

"Kwa kweli uongozi wa urais nchini pasina kuwepo wa ubunge hauwezi kulisaidia pakubwa taifa hili kuimarika. Kumekuwa na dhana kuwa vyama vya kisiasa hujihusisha na wizi wa kura za kitaifa bila kuzingatia iwapo wanapata viti vingi hasa vya ubunge mashinani," alisema Kiangoi.