Spika wa Bunge la kaunti ya Nakuru Susan Kihika amemshtumu mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri kwa kile ametaja ni kuingilia maswala ya binafsi ya familia ya marehemu Kimani Kihika kuhusiana na urithi wa mali.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya wajane saba wa marehemu Kihika kumshtumu spika Kihika kwa madai kwamba anatumia nguvu alizo nazo kurithi mali ya marehemu.
Wajane hao ni Margaret Wambui, Jane Wanjiru, Mary Wangari, Winnie Wanjeri, Charity Nyambura, Miriam Warau na Lucy Wangari.
Na akijibu shtuma hizo katika kikao na wanahabari siku ya Ijumaa mjini Nakuru, Kihika alisema ni makosa kwa maswala ya familia kuingiliwa.
Wakati huo huo, Spika Susan Kihika maarufu kama "Iron Lady" amesema kuwa familia ya Marehemu Kihika haijawai kuwa na mzozo baina yao hadi pale baadhi ya wale ametaja ni wanasiasa kuingilia maswala ya urithi wa mali ya familia hiyo.