Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kijana mmoja amefikishwa mahakamani kujibu shtaka la kumuibia mwanajeshi.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatano kuwa mnamo Novemba 21, 2015, mshtakiwa, Mohamed Juma Rajab, anadaiwa kuiba simu yenye thamani ya shilingi elfu 13 na kitambulisho cha jeshi cha Lparun Jackson akiwa amejiahami kwa kisu katika eneo la Mtongwe, huko Likoni.

Wakati huo huo Rajab amekabiliwa na shtaka la kupatikana na sare za polisi wa magereza kinyume cha sheria.

Rajab alikanusha mashtaka yote mbele ya hakimu Julius Nang’ea.

Mahakama ilimtoza dhamana ya Sh500,000 na mdhamini wa kiasi sawa.

Kesi hiyo itasikilizwa Januari 2, 2016.