Share news tips with us here at Hivisasa

Kijana mwenye umri wa makamo amefungwa miaka 3 gerezani kwa madai ya kumuibia mtalii.

Swaleh Arafat alikamatwa Januari 3, 2016 katika eneo la Fort Jesus kwa madai ya kuiba simu na kamera yote ikiwa ni mali ya thamani ya Dolla 1000 sawia na shilingi 102,390 za Kenya ikiwa ni mali ya raia wa Uchina Li Ying.

Mshitakiwa alikiri kutekeleza wizi huo siku ya Jumatatu mbele ya hakimu wa mahakama ya Mombasa, Richard Odenyo.

Swaleh yuko na siku 14 za kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.