Kijana wa makamo alifungwa miaka mitatu gerezani kwa kosa la wizi.
Kati ya Juni 19,2010 na Agosti 31,2010, Loureth Makau philip akiwa mfanyikazi katika duka la Auto selection katika barabara ya Heile Sallaise, anadaiwa kumuibia muajiri wake Jaudim Mohamed Kassim kima cha shilingi 200,000.
Akitoa hukumu ya kifungo hicho siku ya Jumatatu, hakimu Richard Odenyo alisema kuwa hatua hiyo itakuwa funzo kwa wengine wanaojihusisha na wizi.
Loureth yuko na siku 14 za kukata rufaa.