Kijana wa miaka 20 mjini Eldoret aljitoa uhai alipokuwa akijaribu kutoroka maafisa wa polisi waliotaka kumtia mbaroni hapo Jumatano.
Inadaiwa kuwa kijana huyo alikuwa akitafutwa na polisi kwa madai ya kushiriki uhalifu. Kijana huyo ambaye jamii yake bado haijajitokeza alijitoa uhai alipokuwa akitoroka kupitia kwa dirisha kutoka katika gorofa ya pili katika jumba la Veecam mjini humo.
Kisa hicho kilitokea wakati maafisa wa polisi ambao walikuwa wakimsaka walipomfuata hadi katika chumba hicho na kumkuta akifanya mazoezi ya vyungo katika ukumbi wa mazoezi ya vyungo ya Veecam Gym.
Kwa mujibu wa msimamizi wa ukumbi huo Peter Kemboi ni kwamba marehemu alikuwa mwanachama katika ukumbi huo ambapo huja hapo mara kwa mara kwa mazoezi.
Kemboi alisema maafisa wa polisi walifiaka chumbani humo wakimtafuta ambapo aliwaelezea kwamba yuko na anaendelea na mazoezi.
Baada ya polisi kuambiwa hivyo walipiga kambi katika ukumbi huo wakimsubiri amalize shughuli zake.
Kemboi alisema wakati mteja wake alipogundua kuwa maafisa wa polisi walikuwa wakimsubiri ndiposa alipojaribu kutoroka kupitia kwa dirisha na kuruka chini ya gorofa hiyo.
“Jamaa huyo alikuja hapa mwendo wa saa kumi na mbili jioni kwa mazoezi kama kawaida yake,muda mfupi baadaye maafisa wa polisi walifika hapa wakimuulizia” alisema Bw Kemboi
Kemboi alisema alipoambia polisi jamaa huyo yuko anafanya mazoezi polisi waliamua kumsubiri hadi amalize mazoezi yake. Kemboi aliongeza kuwa punde tu jamaa huyo alipogundua kuwa polisi wanamsubiri aliamua kutumia njia ya dharura katika jengo hilo kabla ya kurukia dirishani na kujitupa kutoka katika gorofa ya nne hadi chini.
“Ilikuwa mwendo wa saa tatu usiku tulipokuwa tukimaliza shughuli zetu ndiposa jamaa huyu alipoamua kujitupa chini huenda alikuwa mhalifu kwani hangejitupa chini kama hakuwa mhalifu,” alisema
Kaimu afisa mkuu wa polisi katika kituo cha polisi cha Eldoret Samson Rukunga alidhibitisha kisa hicho.
Rukunga alisema jamaa huyo alikimbishwa katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi MTRH kabla ya kufariki punde tu alipofikishwa hospitalini humo.
Hata hivyo bw Rukunga alikataa kusema lolote iwapo mwendazake alikuwa akituhumiwa kuhusika na uhalifu wa aina yeyote ile.
“Kwa sasa siwezi nikasema lolote kile najua ni kwamba maafisa wangu wanaendeleza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo,” alisema