Share news tips with us here at Hivisasa

Kijana mmoja alikishwa mahakamani siku ya Jumatano kwa madai ya wizi wa kimabavu.

Nasoro Matano, akiwa pamoja na wenzake ambao hawakuwa mahakamani, wanadaiwa kutekeleza uhalifu huo mnamo Disemba 21, 2015 katika mtaa wa Majengo mjini Mombasa.

Mahakama ilielezwa kuwa mtuhumiwa pamoja na wenzake walimuibia Hasnain Gaya, simu za rununu, shilingi 7, 000 na kibeti wakiwa wamejihami kwa visu.

Hakimu katika mahakama ya Mombasa, Diana Mochache alimpa dhamana ya shilingi 500,000 baada ya mtuhumiwa kukana madai hayo.

Kesi hiyo itasikilizwa Machi 16, 2016.