Wanafunzi watano kutoka kijiji cha Nyaronge waliopata alama ya C+ na zaidi kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne na waliokosa nafasi yakujiunga na vyuo vikuu wamepata sababu ya kutabasamu baada baada ya wenyeji wa kijiji hicho kujitolea kuwapa msaada.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea siku ya Jumatatu kwenye hafla iliyochangisha shillingi elfu 700,000, pesa ambazo zitawekwa kwenye akaunti za benki za shule ambazo tayari wanafunzi hao wamepata nafasi, mwenyekiti wa kijiji hicho Abel Nyabuya alisema kuwa karo ya wanafunzi hao italipwa, huku akiwataka wazazi kugharamia chakula pamoja na matumizi ya wanafunzi husika.

“Huu ni mradi wa kupigiwa mfano, na tunawahimiza watoto wetu kutia bidii kwenye masomo yao kwa sababu hatuna vipande vya ardhi kuwagawia, na pesa ambazo tumechangisha hii leo zitalipiwa karo kwenye akaunti za vyuo mbalimbali ambako wanafunzi hawa wamepata nafasi,” alisema Nyabuya.

Nyabuya aliongeza kwa kusema kuwa kijiji hicho tayari kimepokea msaada kutoka kwa wanasiasa na wahisani, huku akisema kuwa msaada huo utafadhili wanafunzi wengine zaidi watakaofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.

“Tungependa kuwashukru baadhi ya wanasiasa na wahisani waliotupa msaada, na ninafikiri kuwa tuna pesa zakutosha zitakazotusaidia kufadhili masomo ya vyuo vikuu kwa wale wanafunzi watakao fanya vizuri kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne mwaka huu,” alisema Nyabuya.

Kufikia sasa wanafunzi wa kwanza kumi walionufaika na mpango huo ulioanzishwa mwaka wa 2011 watakuwa wakifuzu kutoka vyuo mbalimbali mwezi Desemba mwaka huu.