Mwili wa msichana mmoja ulipatikana Ijumaa asubuhi katika mji wa Kisii.
Mwili huo ulipatikana nyuma ya kanisa la Ambassadors for Christ kisii na inashukiwa msichana huyo alinajisiwa kabla ya kuuawa.
Kulingana na walioshuhudia wanasema kuwa msichana huyo alikuwa wa miaka kati ya 13 na 16.
“Ni mtoto mdogo sana ametolewa nguo zote hata ile ya ndani. Amerepiwa hadi damu bado inaendelea kutoka aliharibiwa kabisa. Na wale walitenda kitendo hicho cha unyama mungu atawalaani.” Mkaazi mmoja alisema.
Ni kitendo cha unyama ambacho kimelaaniwa na umati wa wanawake waliofika kushuhudia unyama huo.
“Aki wanaume yaani mtu anafanyia mwingine unyama kama huu na aende kwake akae akule chakula, ni unyama huu na atalaaaniwa maisha yake yote hatapata amani,” mwanamke mmoja alisema kwa uchungu.
Maafisa wa polisi walifika hapo na kuuchukua mwili wa msichana huyo hadi chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya kisii huku uchunguzi ukiendelea.