Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akina mama wote nchini wameshauriwa kuwanyonyesha watoto wao hadi miaka mitatu ili kuzuia kuathiriwa na ugonjwa wa saratani ya matiti.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa ugonjwa wa saratani ya matiti huenea na kuathiri akina mama kwa kutowanyonyesha watoto wao kwa mda mrefu.

Akizungumza na mwandishi huyu wa habari mnamo siku ya Alhamisi katika hospitali ya rufaa na mafunzo iliyoko mjini Kisii Dkt Douglas Mariita, anayesimamia ugonjwa huo wa saratani katika hospitali hiyo, alisema ikiwa akina mama wanahitaji kupunguza viwango vya kuathiriwa na ugojwa wa saratani ya matiti sharti wawanyonyeshe watoto wao kwa miaka mitatu.

Kulingana naye, utafiti unaonyesha kuwa wengi huathiriwa na ugonjwa huo kwa kuwaachisha watoto wao kuwanyonyesha mapema hata kabla ya miaka miwili, jambo ambalo alisema si la kufurahisha katika jamii.

“Naomba akina mama wote ambao wanatarajia kujifungua na wale wako na watoto waweze kuwanyonyesha watoto wao kwa miaka mitatu ili kupunguza viwango vya kuathiriwa na ugonjwa wa saratani ya matiti kwa akina mama nchini,” alisema Dkt Douglas Mariita.

Wakati huo huo, Mariita aliomba watu kupunguza kula nyama, soda, mkate, pombe miongoni mwa vingine vyakula ambavyo huleta saratani kwa mwili.

“Nawashauri wananchi kupunguza kula nyama, pombe na mikate ile iko na sukari nyingi na kila mtu atakapofuata mtindo wa kula chakula, visa vya saratani vitapungua nchini,” aliongeza Mariita.