Kiongozi mmoja wa ngazi ya juu serikalini anayetuhumiwa kushinikiza ukeketaji wa wasichana na kumuoa msichana wa umri wa chini aliachiliwa kwa muda Jumanne, baada ya mahakama ya juu ya mjini Nakuru kurefusha amri iliyotolewa ya kushtakiwa kwake.
Dkt Titus Pirishon Lenyasunya, ambaye ni mkurugenzi mwendeshaji wa kituo cha utafiti wa mifugo, anatuhumiwa kumwoa Melody Lenyasunya, mwenye umri wa miaka 20, na kisha kumkeketa.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena Disemba 15, 2015.
Na katika mahakama iyo hiyo, keshia wa duka la ujumla la Tuskeys Jumanne alishtakiwa kumwibia muajiri wake shilingi milioni 2.7.
Bwana Boniface Kiharie alituhumiwa kuiba kitita hicho mnamo tarehe 20, mwezi Julai kutoka kwa akaunti ya mwajiri wake katika benki ya Diamond Trust mjini Nakuru.
Korti ilifahamishwa kwamba Bwana Kiharie alitumia cheo chake kutoa pesa hizo katika benki hiyo.
Hata hivyo alikanusha mashtaka hayo na akaachiliwa kwa dhamana ya shilingi 500,000 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.