Vijana kutoka wadi ya Kivumbini Nakuru wamepewa changamoto kuhakikisha wanasoma na kufahamu katiba.
Martin Lunalo ambaye ni kiongozi wa vijana katika muungano wa wakaazi sub kaunti ya Nakuru mashariki anasema kuwa ni jambo la kuskitisha kwamba wengi wa vijana hawafahamu yaliyomo kwenye katiba.
"Vijana wengi hawafahamu katiba na wanafaa kuwajibika na kusoma katiba ili waache kutumiwa na baadhi ya wanasiasa"akasema Lunalo.
Wakati huo huo amewataka vijana kutoka wadi ya Kivumbini Nakuru kujisajili kama wapiga kura ili kushiriki maamuzi ya kaunti na taifa kwa jumla.
"Vijana wasipochukua vitambulisho na kadi za kura itakuwa vigumu sana kwao kushiriki maamuzi," aliongeza Lunalo.
Alikuwa akizungumza wakati wa mahojiano mtaani Greenview Kivumbini Nakuru.