Mbunge wa Naivasha John Kihagi amesema kuwa wawekezaji kutoka Uchina wamekubali kujenga kiwanda cha kupakia samaki mjini Naivasha.
Kihagi amesema kuwa kiwanda hicho kitasaidia pakubwa katika kuwapa ajira vijana na vilevile kuimarisha sekta ya uvuvi katika eneo LA Naivasha. Akiongea Ijumaa mjini Naivasha, Kihagi amesema kuwa kiwanda hicho kitaanza kujengwa mwaka 2016.
"Tumepata wawekezaji kutoka uchina ambao wako tayari kuwekeza hapa Naivasha kwa kujenga kiwanda cha kupakia samaki.Hii itatusaidia kwa sababu vijana na kina mama watapata ajira na pia uchumi wa mji wetu itaimarika,"alisema kihagi.
"Wavuvi watanufaika pia kwa sababu watapata solo la tayari kwa samaki wao na hii itawaepushia hasara," aliongeza.
Aliwataka wavuvi kuimarisha mbinu zako za uvuvi ili kunufaika na kiwanda hicho.
Aidha Kihagi aliwataka wakaazi wa Naivasha kukumbatia kilimo cha samaki akisema kuwa kitawafaidi pakubwa.
"Hatuwezi tegemea ziwa Naivasha pekee na ni vyema tuanze kilimo cha samaki mashambani mwetu ili tuhakikishe kuwa kiwanda kitakachojengwa kina samaki wakutosha,"akasema.