Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Joseph Arap Kabii sasa ndiye mwenyekiti mpya wa chama cha waalimu cha Knut tawi la Nakuru baada yake kupata kura 2,218 kwenye uchaguzi wa viongozi wa chama hicho tawi la Nakuru uliofanyika Alhamisi hii ya tarehe 11 Februari katika shule ya upili ya Afraha mjini Nakuru.

Hayo ni kwa muujibu wa matokeo ambayo yametolewa na wizara ya leba kwenye kaunti ya Nakuru iliyosimamia shughuli hiyo.

Joseph Arap Kabii alimshinda mpinzani wake wa karibu George Mutura Mungai aliyepata kura 1,348 , aliyekuwa akishikilia kiti hicho hapo awali .

Kwa upande mwingine, Kaburi Kuria alipata kiti cha naibu mwenyekiti baada ya kuzoa kura 2,160 huku akimshinda mpinzani wake wa karibu Richard Kirui aliyepata kura 1,725.

Katika uchaguzi huo, James Mungai Muhia naye alipata kiti cha katibu mkuu wa chama hicho tawi la Nakuru baada ya kupata kura 2,210 ambapo alimpiku mshindani wake wa karibu Athony Njoroge aliyepata kura 1,889 huku akichukua kiti hicho kutoka kwa Kuria Njau.

Kiti cha mweka hazina nacho kilijazwa na James Omao aliyepata kura 1,978 huku akimshinda Hotchson Muriuki aliyepata kura 1,234.

Nafasi ya mwakilishi wa wanawake katika chama hicho tawi la nakuru kilijazwa na Chepkoech Alice Bor aliyepata kura 2,281 huku akimshinda mpinzani wake wa karibu kwa jina La Lilian Munene aliyepata kura 2,005.

Tamati………..