Mwanasiasa Koigi wa Wamwere amemkosoa mwenyekiti wa jopo lililoundwa kumchunguza Jaji Philip Tunoi kuhusu madai ya kuchukua hongo ya shilingi milioni mia mbili.
Koigi alisema hatua ya jopo hilo kumpa nafasi jaji Tunoi kuamua iwapo anataka uchunguzi wa kamati hiyo kufanywa mbele ya umma au la ni halifai.
“Mambo ambayo Tunoi anatuhumiwa kufanya yanahusu umma, Tunoi vile vile alikuwa mhudumu wa umma na kwa hivyo hakuna vile maswala hayo yanaweza chunguzwa kisiri,”Koigi alisema.
Mwanaharakati huyo aliongeza kuwa Tunoi anafaa kukabiliwa kisheria kama wakenya wengine ambao hukabiliwa na sharia.
“Wakenya wengine wanapopatikana na madai yoyote huwa hawapewi nafasi ya kuchagua jinsi kesi zao zitaendeshwa. Tunoi ni raia kama wengine na kwa hivyo akabiliwe kawaida,” Koigi aliongeza.