Wanajeshi wa Kenya waliokuwa wameshika doria katika nchi jirani ya Somalia wamo katika hatari kubwa ya kushambuliwa na kundi la waasi la Alshabab.
Mwanajeshi aliyewahi kufanya kazi na jeshi kwa miaka 30 kanali mstaaafu Dickson Swengenyi amesemna kwamba hii ni kutokana hatua ya kutilia maanani sana shambulizi la Alshaabab lililotekelezwa dhidi ya majeshi hayo hivi karibuni .
Kwenye mahojiano Jumatano, alisema kwamba makundi yote ya kigaidi hufurahia sana wanapoona habari za mashambulizi ya kigaidi yakigonga vichwa vya habari .
Ni jambo analosema huwapa motisha wa kuendelea kutekeleza unyama wao.