Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Hatua ya kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi mkuu wa shirika la mafuta nchini kumezua hisia kali kutoka kwa baadhi ya wakazi wa eneo la Pwani, huku wengine wakisema kuwa hatua hiyo huenda ikaendelea kuwatenga wakazi wa maeneo husika kukosa kuipigia kura serikali.

Wakiongea na mwandishi huyo katika jiji la Mombasa siku ya Alhamisi, wakazi hao wamesema kuwa kusimamishwa kazi kwa Sumayya Athman ni wa kuwapoteza baadhi ya wafuasi ambao tayari walikuwa wameanza kuingiliana na upande wa serikali baada ya ziara ya rais Uhuru Kenyatta mwezi jana.

Mmoja wa wakazi hao, Tim Charo, amesema kuwa waziri mpya wa kawi amechukua hatua ambayo itaathiri msimamo na mtazamo mzima wa wakazi ambao wanaitaja hatua hiyo kuwa ya kisiasa, na haifai kamwe kwa wakati huu ambao serikali ya Jubilee inataka kurudishwa mamlakani kufika mwaka ujao.

"Hatua kama hii ya kusimamisha Bi Sumayya ina mwelekeo mbaya wa siasa na inalenga kuwanyamazisha wakazi na kuwanyima wenyeji kuwa na kazi za serikali kama wengine," alisema Charo huku akiwataka viongozi wakuu wa Jubilee kulingalia suala hilo kwa umaakini.

Sumayya anatoka kwenye eneo bunge la Malindi na hatua ya kupewa likizo ya lazima na waziri imetajwa kuwa itapunguza imani na wakazi wa Malindi ambao wanatarajia kupiga kura kwenye eneo bunge hilo mwezi ujao na baadhi ya wachanganuzi wa siasa wamesema kuwa huenda kiti hicho kikashindwa na upinzani.