Share news tips with us here at Hivisasa

Kina mama wanaowekeza pesa zao kwenye kikundi cha ROSEWO (Rongai Social Economical Women Organization) wametakiwa kuzitumia fedha wanazozipokea kutoka kundi hilo ili kujiimarisha kimaisha.

Akizungumza kwenye mkutano wa kikundi hicho wa kufunga mwaka, Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua alisema kwamba akina mama hao wakianzisha biashara hizo watawapa vijana wa Rongai nafasi za ajira.

Kulingana na Kinuthia, ushirika kama huo ni njia bora ya kupunguza ukosefu wa ajira na umaskini nchini, hivyo kuwezesha jamii.

Mkurugenzi wa kikundi hicho Jeniffer Kigen alisema kwamba kikundi kicho kimewawezesha akina mama kujiendeleza maishani kwa kununua mashamba, kuwapeleka watoto wao shuleni, kuongeza mifugo wao na wengine hata kununua magari.

Kukundi hicho kimewasajili akina mama kutoka kaunti ndogo ya Rongai, lakini mwaka ujao wananuia kusajili akina mama wa kaunti zingine ndogo za Nakuru, pia kaunti jirani ya Baringo.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Naibu Gavana wa Kaunti ya Nakuru Joseph Ruto, Mwakilishi mteule wa chama cha URP Irene Jebichi, na Mwakilishi wa Subukia Peter Njoroge.