Ni rasmi sasa kuwa mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani hatajihusisha tena katika miradi ya mrengo wa upinzani Cord, wala kuwania kiti cha ubunge cha eneo hilo kupitia mrengo huo.
Mwashetani alisema haya alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Lunga Lunga na kusema kuwa tokea aanze kushirikiana na serikali ambayo imeundwa na mrengo wa JAP, maendeleo mengi yametekelezwa katika eneo bunge lake.
“Kupitia kwa Rais Uhuru Kenyata, tayari nimepokea million 450 za kuanzisha mradi wa kuleta maji katika eneo lote la Lunga Lunga, jamani si maendeleo haya?”aliuliza mbunge huyo.
Aidha, Mwashetani amesema kuwa wakati wa kuwa katika upinzani na kulalamika kila siku kuhusu kuibiwa kura ulikuwa uimepitwa na wakati.
Mbunge huyo aliyeteuliwa kwa chama cha Ford Kenya, ambacho ni chama moja ya muungano wa Cord, alitimuliwa kutoka kamati ya bunge kuwakilisha mrengo huo baada ya kuasi chama.
Picha: Mbunge wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani na Naibu Rais William Ruto. Huenda Mwashetani amekigura chama cha Cord na kujiunga na JAP. Thestar.co.ke.