Lita mia mbili za pombe haramu aina ya kangara zimepatikana na washukiwa wawili kutiwa mbaroni katika eneo la Katine kaunti ndogo ya Matungulu baada ya msako dhidi ya pombe haramu kuendeshwa na Chifu wa kata ya Tala Pius Nzioka. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Chifu Nzioka akizungumza na wanahabari alisema kuwa yeye pamoja na manaibu wa chifu wa Kata ndogo za Katine na Kyaume pamoja na maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Tala waliendesha msako huo usiku wa kuamkia leo.

Alisema kuwa watafanya juu chini kuhakikisha kuwa pombe haramu imeisha katika eneo hilo pale uko kwa wingi. 

Aisha aliwashukuru wakaazi kwa kuwafahamisha kuhusu uuzaji huo wa pombe haramu. 

"Baada ya kupata ripoti kutoka kwa wakaazi nilifaamisha maafisa wa polisi pamoja na manaibu wangu pale tuliwafumania washukiwa na kupata lita 200 za pombe hio, alisema Nzioka. 

Vilevile mwanamke mmoja wa umri wa makamo anaendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi ha Ndonyo Sabuk baada ya kukamatwa na lita Thelathini za pombe haramu katika msako ulioendeshwa na wanachama wa nyumbakumi wakiongozwa na mwenyekiti wao Jeremiah Kioko katika eneo la Kyanzavi. 

Washukiwa hawa wote wanatarajiwa kufikishwa kortini hivi leo kujibu mashtaka.