Share news tips with us here at Hivisasa

Afisa wa afya ya umma katika kaunti ya Nakuru Samuel Kingo’ri amedhibitisha kuwa amewatuma maafisa wa afya ya umma baada ya kuripotiwa mkurupuko wa ugunjwa wa kipindupindu katika shule ya wasichana ya Naivasha mapema.

Kingori amesema kuwa wanafunzi waliokimbizwa hosipitalini baada ya kukumbwa na maumivu ya tumbo wamedhibitishwa kuwa na kipindupindu.

Akiongea Jumatano katika shule hiyo, afisa huyo alisema kuwa mkurupuko huo ulitokana na maji ya kunywa yaliochanganyikana na maji chafu.

“Ni kweli kulitokea shida hapa na tumegundua kuwa shida ilikuwa ni kipindupindu na tuafanya kila tuwezalo kurejesha hali kuwa ya kawaida,” akasema

“Tumehakakisha kuwa wanafunzi wanapata maji safi ya kunywa na kuwaweka maafisa wetu hapa hadi pale hali itakaporejea kuwa ya kawaida,” King'ori alisema.

Kingori aliwata wazazi wa wanafunzi katika shule hiyo kutobabaika na kuwahakikishia kuwa watoto wao wako salama.

“Nataka kutoa ujumbe kwa wazazi wasiwe na wasiwasi na watulie kwani watoto wao wako salama kabisa,” King'ori alisema.

Aidha Kingori ametoa agizo kwa usimamizi wa shule hiyo kuhakikisha kuwa chakula wanachokula wanafunzi kimepikwa vizuri ili kuepusha madhara zaidi.