Maafisa wa tume huru na mipaka nchini IEBC katika wadi ya Gesima ambao wanafanya usajili wa wapiga kura wamelaumiwa kwa kuhamia vituo vingine bila kuwajulisha wakazi wanakoenda kufanya usajili huo.
Hii ni baada ya kubainika kuwa maafisa hao huamia vituo tofauti tofauti bila kuwajulisha wakazi wanakoenda kufanya usajili huo baada ya kila siku mbili
Wakizungumza siku ya Jumanne katika wadi ya Gesima, wakazi wa wadi hiyo wakiongozwa na Wycliffe Maroko na George Makori walisema wakazi wengi hawatajiandikisha kama wapiga kura maana hawajui kwa kujiandikia kwani maafisa wa IEBC huendelea kuhamia vituo vingine bila wakazi kujua.
Katika wadi ya Gesima, wapiga kura watakuwa wachache sana maana wengi hawajui kwa kujiadikisha. Tunaomba maafisa wa IEBC kupasha habari kwa wakazi, ni siku gani watafanya usajili katika kituo flani ili kuwa rahisi kwa wakazi kujiandikisha kama wapiga kura,” alisema Maroko.
Katika kaunti ya Nyamira, imesemekana kuwa usajili wa wapiga kura uko katika kiwango cha chini ikilinganishwa na sehemu zingine, jambo ambalo si la kufurahisha.