Wahudumu wa kushughulikia usafi mjini Kisii katika wameombwa kuondoa taka kwa wakati unaofaa ili kuboresha mazingira ya wakazi mji humo.
Wahudumu wa matatu katika steji mjini Kisii na wafanyibiashara wengine mjini humo wamelalamikia hali ya wafanyikazi hao wa usafi kuchelewa kuondoa taka zinazorundikwa kwenye steji hiyo ya magari mjini Kisii .
Wakiongea mjini Kisii mnamo siku ya Alhamisi, wahudumu wa matatu mjini humo na wafanyibiashara wengine walikiri kuwa wanasumbuliwa na harufu mbaya inayotokana na taka zinazochelewa kuondolewa katika steji hiyo kila wakati.
Kulingana na Dancan Oigo, dereva wa gari mjini Kisii, mabaki ya uchafu wa kila aina hutupwa katika steji hiyo na huoza haraka, na hivyo kubadilisha hewa na kuchangia mazingira machafu.
“Ikiwa wafanyikazi wa kuondoa uchafu hapa mjini Kisii wanataka kuimarisha na kuboresha mazingira hapa sharti wawajibikie kazi yao kikamilifu kwa wakati unaofaa,” alisema Oigo.
Wakati huo huo, wale wanaofanya biashara tofauti mjini Kisii nao wamesema taka zinapokaa kwa muda mjini humo husababisha wateja kupungua kufuatia mazingira mabaya.
Baada ya malalamishi hayo kwa maafisa wa kuondoa taka zilizorundikana, pia waliwataka wenzao kuhakikisha kwamba wanatupa uchafu katika maeneo yaliyotengwa badala ya kutegemea wahumu wa kufanya usafi.